




Welcome to
Simba Sport Club



October 01, 2016
Kichuya
The King
Mshambuliaji huyo aligundua maisha yake yamebadilika baada ya kurejea kwao Morogoro, mara tu baada ya mechi ya Yanga dhidi ya Simba ambayo yeye alifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho na matokeo kuwa 1-1.
Kichuya kama kama mfalme, kwani hats madereva taxi na wale wa bodaboda hawataki malipo wanapomchukua.
Inaonekana watu wa Morogoro hata wasio mashabiki wa Simba wanajivunia kutokana na kazi nzuri anayoifanya.
Kichuya amekuwa na mafanikio makubwa katika mechi chache tu alizoichezea Simba kutokana na mchango wake mkubwa katika upachikaji mabao pamoja na kutoa pasi.
Hata hivyo, Kichuya amekuwa akisema kwamba hawezi kubweteka hata kidogo kutokana na namna watu wanayoonyesha kumjali badala yake ataongeza juhudi zaidi.

October 04, 2016
Simba Sc On Field
Simba Sport Club
Baada ya mechi yake dhidi ya watani wake Yanga, Simba imeendelea na mazoezi leo kujiandaa na mechi ijayo dhidi ya Mbeya City.
Kikosi cha Simba chini ya Kocha Joseph Omog kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi enero la Shekilango, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Simba inajiandaa na mechi ya ugenini dhidi ya Mbeya City ambayo inatarajiwa kuwa ngumu kwao kwa kuwa Mbeya City itakuwa nyumbani na inahitaji pointi tatu.
â—„
1 / 1
â–º